• HABARI MPYA

  Saturday, April 16, 2016

  SAMATTA KAMA RONALDO! APIGA TENA BAO GENK YASHINDA 2-1 UGENINI

  Na Mwandishi Wetu, WAREGEM 
  NYOTA ya Nahodha wa Tanzania, Mbwana Samatta imeendelea kung’ara Ulaya baada ya leo kuifungia tena klabu yake, KRC Genk katika ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya wenyeji SV Zulte-Waregem.
  Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji uliofanyika Uwanja wa Regenboogstadion mjini Waregem, Samatta alifunga bao la kwanza dakika ya saba tu kwa kichwa akimalizia krosi ya mkongwe wa umri wa miaka 25, Mbelgiji Thomas Buffel.
  Beki wa Kongo mzaliwa wa Ufaransa, Marvin Baudry akajifunga katika harakati za kuokoa dakika ya 15 kuipatia Genk bao la pili, kabla ya mshambuliaji Msenegali, M'Baye Leye kuifungia SV Zulte-Waregem bao la kufutia machozi kwa penalti dakika ya mwisho ya kipindi cha kwanza.
  Mbwana Samatta (wa pili kulia) akipongezwa na wenzake baada ya kufunga bao la kwanza

  Hilo linakuwa bao la nne kwa Samatta katika mechi tisa alizocheza tangu ajiunge na Genk Januari mwaka huu akitokea TP Mazembe ya DRC. 
  Mabao mengine alifunga katika ushindi wa 4-0 na 4-1 dhidi ya KV Oostende na 3-2 dhidi ya Club Brugge.
  Kikosi cha Genk kilikuwa; M. Bizot, C. Kabasele, S. Dewaest, J. Uronen, T. Castagne, O. Ndidi, Pozuelo, N. Kebano/ R. Malinovskiy  dk80, T. Buffel, M. Samatta na L. Bailey.
  SV Zulte-Waregem; K. Steppe, H. Dalsgaard, B. Verboom, M. Baudry, A. Diallo/ F. Mendy dk46, O. Kaya, A. Cordaro, S. De Ridder/J. Benteke dk76, S. Meite, M. Leye na N. Storm/ S. Buyl dk74.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA KAMA RONALDO! APIGA TENA BAO GENK YASHINDA 2-1 UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top