• HABARI MPYA

  Saturday, April 02, 2016

  RONALDOOOO, BARCA WAKAA CAMP NOU…MESSI, NEYMAR SUAREZ ‘NYWIII’

  REAL Madird imefuta uteja kwa wapinzani wao wa kudumu, Barcelona baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 usiku huu Uwanja wa Nou Camp katika mchezo wa La Liga, yaani Ligi Kuu ya Hispania.
  Katika mechi hiyo ya kwanza ya El Clasico kwa Zinedine Zidane kama kocha, mabao ya Real Madrid yamefungwa na Mfaransa Karim Benzema na Mreno, Cristiano Ronaldo, wakati la Barca limefungwa na Gerard Pique.
  Kwa ushindi huo pia, Real imezima wimbi la mechi 39 la Barca bila kufungwa.

  Ronaldo aliwachambua Javier Mascherano (kushoto) na Gerard Pique kabla ya kufunga bao la ushindi 
  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Baada ya dakika 45 kumalizika bila ya timu hizo kufungana, mapema kipindi cha pili, Pique alianza kuifungia Barca dakika 56 kwa kichwa akimalizia kona iliyochongwa na Ivan Rakitic.
  Iliwachukua dakika sita tu Real kusawazisha kupitia kwa Karim Benzema kwa shuti la kisarakasi 
  Akimalizia krosi ya Mjerumani, Toni Kroos ambayo ilikaribia kuzuiliwa na walinzi wa Barca.
  Gareth Bale akaifungia bao Real dakika ya 82 kwa kichwa baada ya pasi ndefu ya juu ya Ronaldo, lakini refa akakataa.
  Real ikampoteza Nahodha wake, Sergio Ramos aliyetolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 83, baada ya kumchezea rafu Luis Suarez.
  Pamoja na kubaki pungufu, Real iliendeleza bidii na mchezo wa kasi, hatimaye Mwanasoka Bora wa zamani wa dunia, Cristiano Ronaldo baada ya kukosa mabao mawili ya wazi, akawainua vitini mashabiki wa timu yake kwa kufunga bao zuri la ushindi dakika ya 85.
  Ronaldo alifunga bao hilo baada ya kuituliza vizuri kifuani krosi ya Bale na kumgeuza Pique kabla ya kumlamba chenga Javier Mascherano na kumchambua kipa Bravo. 
  Kocha Luis Enrique wa Barca aliyechezea timu zote hizo enzi zake hakuamini macho yake kama anapoteza mchezo nyumbani, huku kiungo wa zamani wa Real, Zidane akiruka kwa shangwe la kuzima ubabe wa timu ya Katalunya, tena Camp Nou. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDOOOO, BARCA WAKAA CAMP NOU…MESSI, NEYMAR SUAREZ ‘NYWIII’ Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top