• HABARI MPYA

    Friday, April 08, 2016

    LIVERPOOL YABISHA HODI NUSU FAINALI ULAYA

    LIVERPOOL imejiweka kwenye mazingira mazuri ya kwenda Robo Fainali ya UEFA Europa League baada ya kulazimisha sare ya 1-1 ugenini na Borussia Dortmund Uwanja wa Signal Iduna Park.
    Na Liverpool inayofundishwa na kocha wa zamani wa Borussia, Jurgen Klopp ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Divock Origi dakika ya 36, kabla ya Mats Hummels kuwasawazishia wenyeji dakika ya 48.
    Sasa Liverpool itahitaji hata sare ya 0-0 nyumbani Uwanja wa Anfield Aprili 14 ili kusonga mbele.
    Mfungaji wa bao la Liverpool, Divock Origi akiangalia mawinguni kushangilia baada ya kufunga PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    Mechi nyingine za Robo Fainali ya michuano hiyo leo, Villarreal imeshinda 2-1 dhidi ya Sparta Prague, mabao yote yakifungwa na Cedric Bakambu dakika ya tatu na 63, huku la wageni likifungwa na Jakub Brabec dakika ya 49 Uwanja wa El Madrigal.
    Sporting Braga imefungwa 2-1 nyumbani na Shakhtar Donetsk Uwanja wa Manispaa mjini Braga. Mabao ya Shakhtar yamefungwa na Yaroslav Rakitskiy dakika ya 44 na Facundo Ferreyra dakika ya 75, wakati la wenyeji limefungwa na Wilson Bruno Naval Costa Eduardo dakika ya 89.  
    Athletic Club nayo imefungwa 2-1 nyumbani na Sevilla Uwanja wa San Mames. Mabao ya Sevilla yamefungwa na Timothee Kolodziejczak dakika ya 56 na Vicente Iborra dakika ya 83, wakati la wenyeji limefungwa na Aritz Aduriz Zubeldia dakika ya 47. Timu zote zinatarajiwa kurudiana Alhamisi ijayo, Aprili 14.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LIVERPOOL YABISHA HODI NUSU FAINALI ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top