• HABARI MPYA

  Thursday, April 07, 2016

  DK MATANDIKA ASIMAMISHWA KAZI TFF AKIHUSISHWA NA 'FIGISU'

  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limemsimamsisha kazi kazi kwa muda usiojulikana Juma Matandika 'Dk. Mata', Msaidizi wa Rais Jamal Malinzi, ili kupisha uchunguzi wa sakata la kuomba rushwa ya Sh. Milioni 10 kuisaidia timu moja ya Daraja la Kwanza.
  Taarifa ya TFF jioni ya leo imesema kwamba Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa amemsimamisha kazi Matandika kupisha kuhusu tuhuma za hadhi za wachezaji .
  Hatua hii imechukuliwa kwa mujibu wa ibara ya 266,267 na 268 ya Kanuni za Utumishi za TFF toleo la mwaka 2015.
  Juma Matandika (kulia), Msaidizi wa Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kushoto) amesimamishwa kazi 

  Hamkani si shwati TFF, baada ya kuvuja kwa sauti za maofisa wa shirikisho hilo wakiomba rushwa ya Sh. Milioni kutoka kwa viongozi wa timu moja ya Daraja la Kwanza ili waisaidie kupanda Ligi Kuu.
  Na jana TFF imetoa tamko la kusikitishwa na taarifa hizo na kuahidi kuwachukuliwa hatua kali maofisa wake waliohusika, ingawa imesema taarifa hizo hazihusiani na kesi ya kupanga matokeo iliyoamuliwa Aprili 3.
  TFF imesema kwanza inachunguza kubaini uhalisia (authenticity) wa taarifa hizo na itachukua hatua kali sana kwa watumishi wa shirikisho na viongozi wa timu husika watakaobainika kushiriki vitendo vilivyo kinyume na maadili ya mpira wa miguu.
  Tayari Kaimu Mkurugenzi wa Mashindano TFF, Martin Chacha, mmoja wa watuhumiwa ameacha kazi tangu juzi.
  Katika barua yake aliyomwandikia Katibu Mkuu wa TFF, Chacha amesema amepata majukumu mapya ya kikazi ambayo pamoja na majukumu ya kifamilia yatamfanya akose muda wa kutumika vema katika nafasi yake katika Shirikisho
  Chacha alijiunga na TFF Julai 2014 kama Ofisa Mashindano na baadaye kuteuliwa kukaimu nafasi ya Mkurugenzi wa Mashindano, kufuatia aliyekuwa anashikiria nafasi hiyo Boniface Wambura kuteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DK MATANDIKA ASIMAMISHWA KAZI TFF AKIHUSISHWA NA 'FIGISU' Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top