• HABARI MPYA

  Friday, April 15, 2016

  LIVERPOOL NA VILLARREAL NUSU FAINALI EUROPA LEAGUE, WANAANZIA UGENINI TENA

  TIMU ya Liverpool ya England itamenyana na Villarreal ya Hispania katika Nusu Fainali ya Europa League 2016. 
  Wekundu hao wa Anfiled walifuzu kimiujiza jana wakiitoa Borussia Dortmund katika Robo Fainali kwa bao la kichwa dakika ya mwisho la Dejan Lovren na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 5-4.
  Nusu Fainali nyingine Sevilla itamenyana na  Shakhtar Donetsk.
  Beki wa kati wa Liverpool, Dejan Lovren (katikati kulia) akishangilia baada ya kuifungia bao la ushindi timu yake jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Kama ilivyokuwa katika mechi ya Dortmund, Jurgen Klopp atachezea mechi ya marudiano Merseyside, huku Liverpool ikisafiri kwenda Uwanja wa El Madrigal kwa mchezo wa kwanza.
  Mchezo wa kwanza wa Shakhtar Donetsk dhidi ya Sevilla utachezwa Ukraine na marudiano yatakuwa Uwanja wa Ramon Sanchez Pizjuan. 
  Mechi za kwanza Nusu Fainali zitachezwa Aprili 28, wakati marudiano yatakuwa Mei 5 na fainali itachezwa Uwanja wa St Jakob-Park mjini Basle, Uswisi Mei 18.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL NA VILLARREAL NUSU FAINALI EUROPA LEAGUE, WANAANZIA UGENINI TENA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top