• HABARI MPYA

    Tuesday, April 19, 2016

    KIUNGO MBEYA CITY ALALAMIKA 'KUDHULIMIWA' MABAO LIGI KUU

    Na Doreen Favel, MBEYA
    KIUNGO chipukizi wa Mbeya City FC, Rafael Daudi Alpha (pichani kulia) amesema anashangaa hatajwi katika orodha ya wafunga wa mabao mengi kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wakati hadi sasa ana mabao sita.
    Amesema anashangaa wakati wote orodha ya wafungaji wa mabao mengi wa Ligi Kuu inapotolewa jina lake limekuwa haliorodheshwi hata kwenye tovuti ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
    "Mimi nimefunga mabao sita, lakini mara zote nimekuwa siwekwi kwenye orodha ya wafungaji wakati wachezaji wengine waliofunga sawa na mimi wanatajwa kila mara," amesema kinda huyo wa miaka 21.
    Hata hivyo, nyota huyo aliyecheza mechi zaidi 23 msimu huu Mbeya City, amesema hiyo haimkatishi tamaa kuendelea kufanya kazi yake kwa nguvu zote kuhakikisha anaisaidia timu yake ibaki kwenye Ligi Kuu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIUNGO MBEYA CITY ALALAMIKA 'KUDHULIMIWA' MABAO LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top