• HABARI MPYA

    Saturday, April 02, 2016

    KIPORO CHA YANGA NA MTIBWA CHARUDISHWA KWENYE FRIJI

    SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF) limekubali kuisogeza mbele mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya mabingwa watetezi, Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar iliokuwa ichezwe Jumatano (Aprili 6, 2016) na badala yake itapigwa Aprili 16 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Hiyo inafuatia malalamiko ya Yanga kupangiwa mechi tatu ndani ya wiki moja kabla ya kumenyana na Al Ahly ya Misri Jumamosi ijayo katika Ligi ya Mabingwa Afrika. 
    Kikosi cha Yanga kilichomenyana na Al Ahly mwaka 2014 

    Maana yake, Yanga SC watashuka dimbani leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kumenyana na Kagera Sugar ya Bukoba katika mfululizo wa Ligi Kuu na baada ya hapo watakwenda kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya Al Ahly mwishoni mwa wiki.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE leo, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Murro amesema kwamba mechi hiyo imeondolewa na badala yake itachezwa Aprili 16, kama ilivyopangiwa na Shirikisho hilo.
    Alisema kwa matokeo hayo, kikosi hicho baada ya mchezo wa leo dhidi ya Kagera Sugar, wataendelea kujifua kujiandaa na mechi dhidi ya Al Ahly iliyopangwa kufanyika Aprili 9 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Kwa upande wake, Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi amesema wao wamekataa kuahirishiwa mchezo wao na Ndanda FC na watashuka dimbani Aprili 6 kumalizia kiporo hicho.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIPORO CHA YANGA NA MTIBWA CHARUDISHWA KWENYE FRIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top