• HABARI MPYA

    Tuesday, March 08, 2016

    ULIMWENGU FITI KABISA KUICHEZEA STARS DHIDI YA CHAD, MAZEMBE YAMRUHUSU KUJA DAR

    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu (pichani kushoto) yuko fiti kabisa sasa na atakuja nchini kuichezea nchi yake mechi mbili za Kundi G kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani.
    Na klabu yake, Tout Puissant Mazembe imemruhusu kuja Dar es Salaam kuugana na Taifa Stars kwa ajili ya michezo miwili ya nyumbani na ugenini dhidi ya Chad.
    TPM imemuambia Ulimwengu, maarufu kama Rambo mbele ya mashabiki wa Lubumbashi kwamba atakwenda Dar es Salaam mara tu baada ya mchezo wa marudiano wa Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya St George ya Ethiopia Jumapili ya Machi 20 mjini Lubumbashi.
    Taifa Stars watakuwa wageni wa Chad Jumatano ya Machi 23 mjini N'Djamena, kabla ya timu hizo kurudiana Machi 28 mjini Dar es Salaam.
    Ulimwengu akiumia mguu akiichezea Mazembe dhidi ya St Eloi Lupopo Februari 17, mwaka huu katika Ligi Kuu ya DRC timu hizo zikitoka sare ya 0-0 na akacheza kwa dakika 12 za mwisho huku akichechemea Februari 20 katika mchezo wa Super Cup ya CAF dhidi ya Etoile du Sahel ya Tunisia mjini Lubumbashi, wenyeji wakishinda 2-1.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ULIMWENGU FITI KABISA KUICHEZEA STARS DHIDI YA CHAD, MAZEMBE YAMRUHUSU KUJA DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top