• HABARI MPYA

  Tuesday, March 08, 2016

  KALABA BADO NAHODHA CHIPOLOPOLO, AKIAMUA KUMPA BEJI KATONGO YEYE TU

  KIUNGO Rainford Kalaba bado Nahodha wa timu ya taifa ya Zambia, kwa mujibu wa kocha George Lwandamina.
  Lwandamina amemaliza utata ulioibuka juuya Unahodha wa Zambia, kufuatia mshambuliaji mkongwe, Christopher Katongo kurejea kikosini kwa ajili ya michezo ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2017 ya Kundi E dhidi ya Kongo-Brazzaville nyumbani Machi 23 na ugenini Machi 27.
  Kiungo huyo wa TP Mazembe amekuwa Nahodha wa Zambia tangu Januari mwaka jana baada ya Katongo kuondolewa kwenye timu Oktoba mwaka 2014 na kocha wa wakati huo, Honour Janza.

  Rainford Kalaba bado Nahodha wa timu ya taifa ya Zambia, kwa mujibu wa kocha George Lwandamina

  "Hadi sasa, Kalaba ni Nahodha. Kurejea kwa hakumaanishi kwamba atakuwa Nahodha, hapana, tunaweza kusema Kalaba atabakia kuwa Nahodha,” amesema Lwandamina.
  "Tutajadili hili tutakapokutana, lakini ni juu ya Kalaba.”
  Katongo alirejea kikosini Zambia Januari mwaka huu wakati alipoiongoza Chipolopolo katika michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) nchini Rwanda mapema mwaka huu, akampokonya beji ya Unahodha kipa wa Zesco United, Jacob Banda.
  Katika michuano hiyo, ambayo Katongo alifunga bao moja pia na kuisadia Zambia kufika Robo Fainali ambako ilitolewa na Guinea.
  "Kama ilivyotokea Chan ambako Jacob alijisikia hawezi kukaa na beji na akampa Katongo,” amesema Lwandamina.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KALABA BADO NAHODHA CHIPOLOPOLO, AKIAMUA KUMPA BEJI KATONGO YEYE TU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top