• HABARI MPYA

    Tuesday, March 08, 2016

    MKWASA AWATEMA NGASSA, CANNAVARO, MSUVA TAIFA STARS, AWAREJESHA KADO NA KAZIMOTO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars amewarejesha kikosini kipa Shaaban Hassan Kado na kiungo Mwinyi Kazimoto Mwitula, huku akiwatema nyota wa Yanga, beki Nadir Haroub 'Cannavaro' na winga Simon Msuva. 
    Mkwasa ambaye pia hajamuita kiungo mshambuliaji wa Free State Stars ya Afrika Kusini, Mrisho Ngassa (pichani) ameita wachezaji 25 kwa ajili ya michezo miwili ya nyumbani na ugenini wa kufuzu Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) mwakani dhidi ya Chad, Machi 23, 2016 mjini Djamena na siku nne baadaye Dar es Salaam.
    Akizungumza na Waandishi wa Habari leo ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ilala, Dar es Salaam, Mkwasa amewaomba wachezaji aliowaita katika kikosi hicho kujiweka fiti katika mazoezi wanayoyafanya katika klabu vyao, kwani hakutakuaw na muda wa kufanya mazoezi kwa ajili ya mchezo huo wa ugenini.
    “Ligi Kuu ya Vodacom, michuano ya klabu Afrika, inachezwa wikiendi ya tarehe 18-20 Machi, hivyo wachezaji wote watakua na majukumu katika timu zao, muda wa kufanya mazoezi kwa pamoja kwa ajili ya mchezo huo hautakuwepo, ndio maana nasisitiza wachezaji niliowachagua wahakikishe wanajilinda wenyewe kwa kuwa fit wanapokuja kwenye safari ya mchezo huo wa machi 23, 2016” alisema Mkwasa

    KIKOSI KAMILI TAIFA STARS;
    Makipa; Aishi Manula (Azam FC), Ally Mustapha (Yanga SC) na Shaaban Kado (Mwadui FC), mabeki; Juma Abdul, Haji Mwinyi, Kevin Yondani (Yanga SC), Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, David Mwantika (Azam FC) na Mohamed Hussein (Simba SC).
    Viungo Himdi Mao (Azam FC), Ismail Juma (JKU), Jonas Mkude, Said Ndemla, Mwinyi Kazimoto (Simba SC), Mohammed Ibrahim, Shizza Kichuya (Mtibwa Sugar), Farid Mussa (Azam FC), Deus Kaseke (Yanga SC).
    Washambuliaji; Mbwana Samatta (Nahodha, KRC Genk Ubelgiji), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), John Bocco (Azam FC), Elias Maguri (Stand United), Jeremia Mgunda (Tanzania Prisons) na Ibrahim Hajib (Simba SC).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MKWASA AWATEMA NGASSA, CANNAVARO, MSUVA TAIFA STARS, AWAREJESHA KADO NA KAZIMOTO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top