• HABARI MPYA

    Wednesday, February 11, 2026

    KIBU DENIS KWAHERI SIMBA SC , AJIUNGA A AL NASR YA LIBYA


    KLABU ya Simba imemtakia kila la heri mshambuliaji wake, Kibu Denis Prosper ambaye anahamia Al Nasr SC ya Libya kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu kwa ada ya uhamisho ya Dola za kimarekani 250,000.
    “Baada ya kuwa sehemu ya kikosi chetu kwa misimu minne na nusu, Kibu Denis ‘Mkandaji’ ameuzwa na sasa anakwenda kuanza maisha mapya nje ya Simba SC,” imesema taarifa ya Simba usiku huu.
    Naye Kibu Denis aliaga baada ya mazoezi ya jana akishukuru kwa muda wote alioitumikia Simba SC na kuitakia kila la heri katika ushiriki wake wa mashindano mbalimbali ishinde mataji na kuwafurahisha mashabiki wake.
    Kibu aliyejiunga na Simba mwaka 2021 akitokea Geita Gold – anakwenda kuungana tena na mshambuliaji wa Kimataifa wa Uganda, Steven Dese Mukwala ambaye alitangulia kusajiliwa Al Nasr.

    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIBU DENIS KWAHERI SIMBA SC , AJIUNGA A AL NASR YA LIBYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top