WENYEJI, Pamba Jiji FC wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Bao pekee la Pamba Jiji FC ambayo kama Namungo FC nayo inamilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza limefungwa na mshambuliaji Mkenya, Mathew Tegisi Momanyi dakika ya 55 ya mchezo huo.
Kwa ushindi huo Pamba Jiji FC inafikisha pointi 23 katika mchezo wa 14 na kusogea nafasi ya pili ikizidiwa pointi nne na JKT Tanzania ambayo pia imecheza mechi moja zaidi, wakati Namungo FC inabaki na pointi zake 20 za mechi 13 nafasi ya tano.



.png)
0 comments:
Post a Comment