• HABARI MPYA

  Wednesday, March 09, 2016

  STRAIKA LA PRISONS LABEBA TUZO YA MCHEZAJI BORA LIGI KUU FEBRUARI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa timu ya Prisons ya Mbeya, Mohammed Mkopi (pichani kushoto) amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa mwezi Februari.
  Mkopi katika mwezi huo uliokuwa na raundi nne, alicheza mechi zote nne za timu yake dhidi ya Mbeya City, Yanga, Mwadui na Mgambo Shooting. Alitoa mchango mkubwa kwa timu yake katika mechi hizo ambapo zote ilitoka sare, hivyo kupata jumla ya pointi nne.
  Katika mechi hizo ambazo Prisons ilifunga mabao matatu, Mkopi alifunga bao moja na kusaidia kupatikana mabao mengine mawili.
  Mshambuliaji huyo ambaye hadi sasa amefunga mabao sita kwenye Ligi hiyo, aling'ara zaidi katika mechi mbili kati ya hizo nne ambapo alichaguliwa kuwa mchezaji bora.
  Mkopi ambaye ni mshambuliaji wa kati alichaguliwa mchezaji bora kwenye mechi dhidi ya Mwadui iliyochezwa mkoani Shinyanga, na ile dhidi ya Yanga iliyofanyika Uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.
  Kwa kunyakua tuzo ya mchezaji bora kwa Februari, Mkopi atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) na wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom.
  Wachezaji bora wa miezi miwili iliyopita ni kiungo Thabani Kamusoko wa Yanga (Desemba 2015), na beki Shomari Kapombe wa Yanga (Januari 2016).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: STRAIKA LA PRISONS LABEBA TUZO YA MCHEZAJI BORA LIGI KUU FEBRUARI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top