• HABARI MPYA

  Wednesday, March 09, 2016

  MKUTANO MKUU TFF MAMBO YAIVA, NGOMA KUPIGWA TANGA JUMAMOSI

  MKUTANO Mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) utafanyika wikiendi hii ya Jumamosi na Jumapili Machi 12 na 13 kwenye ukumbi wa hoteli ya Regal Naivera mjini Tanga.
  Awali, Mkutano huo ilikuwa ufanyike Desemba mwaka jana, lakini ikashindikana kutokana na TFF kutokuwa na fedha.
  Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto, ajenda za mkutano huu ni kwa mujibu wa katiba ya TFF. 
  Mkutano mkuu utahitimishwa kwa uwekaji wa jiwe la msingi la kituo cha kukuza na kuendeleza vipaji vya uchezaji mpira, kituo kitakachojengwa jijini Tanga.
  Wajumbe wa Mkutano Mkuu katika pocha ya pamoja kwenye moja ya mikutano iliyotangulia
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MKUTANO MKUU TFF MAMBO YAIVA, NGOMA KUPIGWA TANGA JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top