• HABARI MPYA

  Wednesday, March 09, 2016

  REFA MDADA WA SIMBA NA YANGA AULA FIFA, APEWA MECHI YA KOMBE LA DUNIA

  REFA wa kike wa Kimataifa wa Tanzania, mwenye beji ya FIFA, Jonesia Rukyaa ameteuliwa kuungana na waamuzi kutoka nchini Kenya kuchezesha mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia kwa Wanawake  wenye umri chini ya miaka 17 (WWC-Q 17) mwishoni mwa mwezi huu.
  Jonesia Rukyaa atakua mwamuzi wa akiba katika mchezo huo kati ya Misri dhidi ya Cameroon utakaochezwa jijini Cairo wikiendi ya tarehe 25,26,27 Machi, 2016.
  Mwamuzi wa kati katika mchezo huo atakua ni Carolyne Wanjala (Kenya), akisaidiwa na Carolyne Kiles (Kenya), Mary Njoroge (Kenya), huku kamisaa wa mchezo huo akiwa ni Leah Annette Dabanga kutoka nchi ya Afrika ya Kati. 
  Jonesiya Rukyaa amejipatia umaarufu baada ya kuchezesha mechi mbili za watani wa jadi, Simba na Yanga nchini, ikiwemo ile ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wiki mbili zilizopita.
  Katika mchezo wake wa kwanza wa Nani Mtani Desemba 13, mwaka 2014, mabao ya Awadh Juma na Elias Maguri yaliipa SImba ushindi wa 2-0, wakati wa Ligi Kuu Februari 20, mwaka huu, mabao ya Donald Ngoma na Amissi Tambwe yaliipa Yanga ushindi wa 2-0.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REFA MDADA WA SIMBA NA YANGA AULA FIFA, APEWA MECHI YA KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top