• HABARI MPYA

  Sunday, March 06, 2016

  SIMBA SC KUREJEA KILELENI LEO? UTAMU WARUDI PALE PALE LIGI KUU

                          P W D L GF GA GD Pts
  Yanga SC 20 14 5 1 46 11 35 47
  Azam FC 20 14 5 1 36 13 23 47
  Simba SC 20 14 3 3 35 13 22 45

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC inashuka dimbani leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kumenyana na Mbeya City katika mchezo ambao ikishinda inapanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Hiyo inafuatia Yanga SC kutoa sare ya 2-2 na Azam FC jana Uwanja wa Taifa na sasa timu zote zinafungana kileleni mwa ligi hiyo, kila moja ikiwa na pointi 47 baada ya kucheza mechi 20. Lakini Simba leo ikicheza mechi ya 21, ikishinda itafikisha pointi 48 na kurejea kileleni mwa ligi hiyo.
  Katika mchezo wa jana uliochezeshwa na refa Kennedy Mapunda, aliyesaidiwa na Frank Komba na Soud Lilla, wote wa Dar es Salaam, hadi mapumziko, Yanga walikuwa mbele kwa mabao 2-1
  Mshambuliaji tegemeo la mabao wa Simba, Hamisi Kiiza leo anatarajiwa kuiongoza tena timu yake katika Ligi Kuu

  Azam FC ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 10, baada ya beki wa Yanga, Juma Abdul Jaffar kujifunga katika jitihada za kuokoaa shuti la mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche.
  Hata hivyo, beki wa kulia, Juma Abdul akasawazisha makosa yake dakika ya 28 baada ya kufunga kwa shuti la umbali wa mita 20 bada ya kukutana na mpira ulioridishwa na beki wa Axam FC, Serge Wawa kufuatia shuti la Amissi Tambwe.
  Mshambuliaji wa Burundi, Tambwe alipokea pasi ya Mzimbabwe, Donald Ngoma ambaye alianzishwia mpira wa kurusha na Mwinyi Hajji Mgwali.
  Zikiwa zimesalia dakika tatu mchezo kuwa mapumziko, mshambuliaji wa Zimbabwe, Donald Ngoma akaifungia Yanga bao la pili kwa kichwa akimalizia pasi ya juu ya Tambwe.
  Kabla ya kumpasia Ngoma, Tambwe alijaribu kufunga mwenyewe baada ya kupokea pasi ya Deus Kaseke, lakini shuti lake liliokolewa na kipa Aishi Manula na kumrudia tena Mrundi huyo, ambaye alimuinulia Donald aliyewainua vitini mashabiki wa Yanga dakika ya 42.
  Kipa Aishi Manula a,ijitahidi kwenda kuokoa mpira huo ukiwa umekwishangia nyavuni, lakiji haujagusa chini – hata hivyo refa Mapunda akawapa Yanga haki yao.
  Kipindi cha pili, Azam FC walirudi kwa bidii kutaka kusawazisha bao, lakini mchezo ukawa wa mashambulizi ya pande zote mbili.
  Hata hivyo, mabadiliko ya kocha Muingereza wa Azam FC, Stewart John Hall kuwaingiza wachezaji wa zamani wa Yanga kiungo Frank Domayo na mshambuliaji Didier Kavumbangu yaliisaidia timu yake kuongeza kasi ya mchezo.
  Na hatimaye Nahodha John Rapahael Bocco akaisawazishia timu yake dakika ya 70 kwa shuti kali akiwa ndani ya boksi, baada ya kupokea pasi ya Kipre Tchetche.
  Kidogo Yanga wakaonekana ‘kupooza’ baada ya bao hilo huku Azam FC wakiendelea kusaka bao la ushindi.
  Kuona hivyom kocha Mholanzi akaamua kuiwekea udhibiti pointi moja, baada ya kumuingiza beki Pato Ngonyani kwenda kuchukua nafasi ya Tambwe dakika ya 82.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC KUREJEA KILELENI LEO? UTAMU WARUDI PALE PALE LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top