• HABARI MPYA

  Sunday, March 06, 2016

  SAMATTA ACHEZA DAKIKA TISA TU, GENK ‘YATAFUNWA’ 2-1 UGENINI NA STANDARD LIEGE

  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana (pichani kushoto) amecheza mechi yake ya nne Ligi Kuu ya Ubelgiji kwa staili ile ile ya kutokea benchi, timu yake KRC Genk ikifungwa 2-1 na Standard Liege ugenini.
  Katika mchezo huo uliofanyiks Uwanja wa Maurice Dufrasne mjini Liege, Samatta aliingia dakika ya 81 kuchukua nafasi ya mfungaji wa bao la Genk, Nikolaos Karelis.
  Karelis alifunga bao hilo dakika ya 42, akimalizia kazi nzuri ya Alejandro Pozuelo, wakati mabao ya wenyeji yalifungwa na Ivan Santini dakika ya 48 na Mamadou Jean-Luc Diarra Dompe dakika ya 69.
  Wiki iliyopita, Samatta alifunga bao lake la kwanza Ligi Kuu ya Ubelgiji, Genk ikishinda 3-2 dhidi ya Clube Brugge.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA ACHEZA DAKIKA TISA TU, GENK ‘YATAFUNWA’ 2-1 UGENINI NA STANDARD LIEGE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top