• HABARI MPYA

  Sunday, March 06, 2016

  SIASIA AITA WACHEZAJI 42 KIKOSI CHA AWALI KWA AJILI YA MECHI NA MISRI

  KOCHA mpya wa Nigeria, Samson Siasia ameita wachezaji 42 katika kikosi chake cha awali kwa ajili ya mchezo wa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2017 dhidi ya Misri baadaye mwezi huu.
  Siasia, aliyechukua nafasi ya mchezaji mwenzake wa zamani wa Super Eagles, Sunday Oliseh aliyejiuzulu wiki iliyopita, ameita wachezaji 20 wanaocheza nje na 22 wanaocheza nyumbani katika kikosi hicho.
  Super Eagles watakuwa wenyeji wa Mafarao katika mchezo wa Kundi G Machi 25, mwaka huu, kabla hawajasafiri kwenda kurudiana nchini mjini Alexandria, Misri siku nne baadaye.
  Kocha wa Nigeria, Samson Siasia ameita wachezaji 42 katika kikosi cha awali kwa ajili ya mechi na Misri

  Wachezaji wa nyumbani wameingia kambini mjini Abuja leo na kesho wataanza mazoezi. Nigeria inaongoza kundi hilo kwa pointi zake sita, ikifuatiwa na Misri yenye pointi nne baada ya mechi mbili za awali, wakati Tanzania yenye pointi moja ni ya tatu na Chad inashika mkia.
  Tanzania na Chad nazo zitamenyana nyumbani na ugenini katika wiki hiyo hiyo ndani ya muda huo huo.
  Kikosi cha Super Eagles ni makipa; Ikechukwu Ezenwa (Sunshine Stars); Olufemi Thomas (Enyimba FC); Emmanuel Daniel (Enugu Rangers), Carl Ikeme (Wolverhampton Wanderers, England); Daniel Akpeyi (Chippa United, Afrika Kusini)
  Mabeki; Kalu Orji Okogbue (Enugu Rangers); Chibuzor Okonkwo (FC IfeanyiUbah); Mathew Etim (Enugu Rangers); Austin Oboroakpo (Abia Warriors); Sincere Seth (Rhapsody FC); Segun Oduduwa (Nath Boys); Chima Akas (Akwa United); Chris Madaki (Kano Pillars); Oke Ogogatewho (Sunshine Stars); Efe Ambrose (Celtic FC, Scotland); Abdullahi Shehu (Uniao da Madeira, Ureno); Elderson Echiejile (AS Monaco, Ufaransa); Stanley Amuzie (Olhanense FC, Ureno); Godfrey Oboabona (Caykur Rizespor, Uturuki) na Kenneth Omeruo (Kasimpasa FC, Uturuki)
  Viungo: Ifeanyi Mathew (Kano Pillars); Usman Mohammed (FC Taraba); Etebo Oghenekaro (Warri Wolves); Yau Hassan (Wikki Tourists); Stanley Dimgba (Warri Wolves), Ogenyi Onazi (SS Lazio, Italia); John Mikel Obi (Chelsea FC, England); Kelechi Iheanacho (Manchester City, England) na Azubuike Okechukwu (Yeni Matalyspor, Uturuki).
  Washambuliaji ni; Ezekiel Bassey (Enyimba FC); Prince Aggrey (Kano Pillars); Bright Onyedikachi (FC IfeanyiUbah); Chisom Chikatara (Abia Warriors); Godwin Obaje (Wikki Tourists); Ahmed Musa (CSKA Moscow, Urusi); Moses Simon (KAA Gent, Ubelgiji); Victor Moses (West Ham United, England); Aminu Umar (Osmanlispor FK, Uturuki); Odion Ighalo (Watford FC, England); Aaron Samuel (CSKA Moscow, Urusi); Alex Iwobi (Arsenal FC, England) na Fanendo Adi (Portland Timbers, Marekani)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIASIA AITA WACHEZAJI 42 KIKOSI CHA AWALI KWA AJILI YA MECHI NA MISRI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top