• HABARI MPYA

  Friday, March 04, 2016

  ROBO FAINALI KOMBE LA TFF; SIMBA WAPEWA COASTAL, YANGA NA NDANDA...AZAM NA PRISONS, PATAMU HAPO!

  ROBO FAINALI KOMBE LA AZAM SPORTS FEDERATON
  Machi 26, 2016
  Geita Gold VS Mwadui FC (CCM Kirumba, Mwanza)
  Machi 31, 2016
  Yanga SC Vs Ndanda FC (Taifa, Dar es Salaam)
  Azam FC Vs Prisons (Azam Complex, Dar es Salaam.
  Aprili 6, 2016
  Simba SC Vs Coastal Union (Taifa, Dar es Salaam)
  Simba itamenyana na Coastal Union Kombe la TFF Robo Fainali

  AZAM FC itamenyana na Tanzania Priaons katika Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup, wakati Simba itamenyana na Coastal Union na Yanga na Ndanda FC.
  Machi 26, 2016 utachezwa mchezo mmoja ambapo Wachimba dhahabu wa Geita Gold watakua wenyeji wa wachimba Almasi wa mkoa wa Shinyanga timu ya Mwadui FC katika uwanja wa CCM Kirumba.
  Alhamisi ya Machi 31, 2016, Young Africans watawakaribisha Ndanda FC katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku timu ya Azam FC wakiwa wenyeji wa maafande wa jeshi la magereza Tanzania Prisons katika uwanja wa Azam Complex Chamazi.
  Mchezo wa mwisho wa robo fainali utachezwa Aprili 6, 2016 kwa Simba SC kucheza dhidi ya Coastal Union katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
  Aprili 7, 2016 itachezeshwa droo ya hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC) mojamoja (live) katika Luninga.
  Bingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho msimu huu, ataiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF CC) 2017.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ROBO FAINALI KOMBE LA TFF; SIMBA WAPEWA COASTAL, YANGA NA NDANDA...AZAM NA PRISONS, PATAMU HAPO! Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top