• HABARI MPYA

  Friday, March 04, 2016

  EBOUE KUREJEA ENGLAND, SUNDERLAND TAYARI KUMSAJILI

  BEKI wa kimataifa wa Ivory Coast, Emmanuel Eboue anaweza kurejea Ligi Kuu ya England, baada ya klabu ya Sunderland kuonyesha nia ya kumsajili.
  Beki huyo wa zamani wa Arsenal amekuwa kivutio kwenye mazoezi ya Sunderland na leo anatarajiwa kusaini Mkataba wa hadi mwishoni mwa msimu.
  Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 32 kwa sasa ni mchezaji huyu baada ya kutemwa na klabu ya Galatasaray mwaka jana. Kwa wiki tatu amekuwa akifanya mazoezi na Sunderland na akacheza dakika zote 90 Jumatatu U21 ya klabu hiyo ikiifunga Leicester City.

  Sunderland inatarajiwa kumsajili beki wa zamani wa Galatasaray, Emmanuel Eboue kwa mkataba wa hadi mwishoni mwa msimu PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  WASIFU WA EMMANUEL EBOUE  

  Mwaka Timu  Mechi Mabao
  2001–2002 ASEC     25- (3)
  2002–2005 Beveren 70- (4)
  2005–2011 Arsenal  132-(5)
  2011–2015 G'tasaray 77-(4)
  Kocha Sam Allardyce aliuangalia mchezo huo wakati kocha wa U21, Andy Welsh alivutiwa na mchango wa mchezaji huyo wa Ivory Coast. 
  "Nilizungumza naye na alisema hizo zilikuwa dakika 90 za kwanza kucheza kwa zaidi ya mwaka," amesema Welsh. 
  "Alionyesha juhudi nzuri na alionekana vizuri wakati mchezo ukiwa mkali. Amekuwa mtu mzuri kwenye chumba cha kubadilishia nguo akiwa na wachezaji nyota nyipukizi, anawasaidia, hivyo sijapata malalamiko yoyote
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: EBOUE KUREJEA ENGLAND, SUNDERLAND TAYARI KUMSAJILI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top