• HABARI MPYA

  Friday, March 04, 2016

  'BABA WAWILI' JUMA KASEJA AENGULIWA SIMBA NA MBEYA CITY, PHIRI ASEMA...

  Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
  KOCHA Mkuu wa Mbeya City FC, Mmalawi Kinnah Phiri amesema kipa Juma Kaseja 'Baba Wawili' (pichani kushoto) hatakuwamo kwenye programu ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Simba SC Jumapili hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kutokana na sababu za kifamilia.
  Muda mfupi uliopita kocha Phiri ameudokeza mtandao huu kuwa ilikuwa waungane na kipa huyo leo asubuhi kwenye kambi ya muda hapa Morogoro lakini imemlazimu kumuongezea muda zaidi wa kukaa  karibu na familia yake ili kushughulikia masuala kadhaa ya kifamilia aliyonayo hivi sasa.
  “Wakati anaondoka Mbeya siku tano zilizopita tulikubaliana kuwa ataungana nasi hapa siku ya leo, nimezungumza nae leo asubuhi kuna mambo muhimu ya kifamilia amenieleza hivyo basi nimeamua kumuongezea siku  kadhaa za kubaki nyumbani kushughulikia  yale yote yaliyopo kwenye familia yake na imani yangu kuwa ataungana na kikosi mara tu tutakaporejea mbeya kujiandaa na mchezo dhidi ya Stand United March 10.
  Juma  Kaseja aliondoka jijini Mbeya mara  baada ya mchezo wa Kombe la FA  dhidi ya Tanzania Prison  uliochezwa kwenye uwanja wa Sokoine kufuatia taarifa njema  ya mkewe kujifungua watoto mapacha.
  Wachezaji wanzeke na uongozi wa City  kwa ujumla unampongeza Juma Kaseja na kumtakia  kila la kheri kwenye malezi ya watoto wake.
  Mbeya City imeweka kambi Morogoro kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba na inatarajiwa kuingia Dar es Salaam kesho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: 'BABA WAWILI' JUMA KASEJA AENGULIWA SIMBA NA MBEYA CITY, PHIRI ASEMA... Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top