• HABARI MPYA

  Wednesday, March 09, 2016

  MAN UTD NA WEST HAM, ARSENAL NA WATFORD, CHELSEA NA...ROBO FAINALI KOMBE LA FA ENGLAND

  RATIBA ROBO FAINALI KOMBE LA FA ENGLAND


  Ijumaa Machi 11, 2016
  ReadingvCrystal PalaceUwanja wa Madejski Saa 4:55 usiku
  Jumamosi Machi 12, 2016
  EvertonvChelseaUwanja wa Goodison ParkSaa 2:30 usiku
  Jumapili Machi 13, 2016

  ArsenalvWatfordUwanja wa Emirates Saa 10:30 jioni
  Manchester UnitedvWest Ham UnitedUwanja wa Old TraffordSaa 1:00 usiku
  Nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney ambaye timu yake itamenyana na West Ham United katika Robo Fainali Kombe la FA England

  BAADA ya kuitoa Hull City, Arsenal itamenyana na Watford katika Robo Fainali ya Kombe la FA England, wakati Manchester United itamenyana na West Ham United.
  Arsenal itacheza nyumbani Uwanja wa Emirates Machi 13, Jumapili wiki hii kama Manchester United ambayo itaikaribisha West Ham Uwanja wa Old Trafford siku hiyo.
  Mechi nyingine za Robo Fainali, Reading itaikaribisha Crystal Palace Uwanja wa Madejski Ijumaa ya Machi 11, wakati Jumamosi ya Machi 12, Chelsea wataifuata Everton Uwanja wa Goodison Park.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UTD NA WEST HAM, ARSENAL NA WATFORD, CHELSEA NA...ROBO FAINALI KOMBE LA FA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top