• HABARI MPYA

    Wednesday, March 09, 2016

    PLUIJM: TUNAKWENDA KUKOMAA NAO APR, HAKUNA KUFUNGWA AMAHORO

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mkuu wa Yanga SC, Mholanzi Hans van der Pluijm amesema kwamba wanakwenda kwenye mchezo mgumu wa ugenini dhidi ya APR, lakini watapambana wasipoteze.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE jana, Pluijm amesema kwamba mchezo huo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika, utakuwa mgumu kwa sababu APR ni timu nzuri.
    “APR ni timu nzuri na watakuwa wamejiandaa vizuri, lakini sisi tuko vizuri, tutakwenda kupambana tusipoteze mchezo, ili tumalizie vizuri mchezo wa nyumbani,”amesema.
    Yanga SC inatarajiwa kuondoka kesho nchini kwenda Kigali, Rwanda kwa ajili ya mchezo huo, unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua.  
    Kocha Hans van der Pluijm (kushoto) akiwa na Msaidizi wake, Juma Mwambusi

    Mechi hiyo inatarajiwa kuchezeshwa na marefa wa Malawi Jumamosi Uwanja wa Amahoro, Kigali Rwanda.
    Duncan Lengani anatarajiwa kupuliza filimbi, wakati washika vibendera watakuwa Clemence Kanduku na Jonizio Luwizi.
    Mchezo wa marudiano wiki moja baadaye Dar es Salaam, utachezeshwa na marefa wa Shelisheli; katiati Bernard Camille na pemebeni watakuwapo Eldrick Adelaide na Gerard Pool.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PLUIJM: TUNAKWENDA KUKOMAA NAO APR, HAKUNA KUFUNGWA AMAHORO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top