• HABARI MPYA

  Saturday, March 12, 2016

  PLUIJM AWAPANGIA APR ‘MIDUME’ ILIYOIFANYA VIBAYA SIMBA DAR

  Na Prince Akbar, KIGALI
  KOCHA Mholanzi wa Yanga SC, ameanzisha kikosi kama ambacho alikitumia kwenye mechi dhidi ya mahasimu, Simba Februari 20, mwaka huu kwa ajili ya mchezo dhidi ya APR jioni ya leo Uwanja wa Amahoro, Kigali.
  Yanga watashuka Uwanja wa Amahoro mjini Kigali, Rwanda kuanzia Saa 10:30 jioni kumenyana na wenyeji, APR katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Na Pluijm amerudisha wachezaji 10 kati ya 11 aliowaanzisha akiwafunga 2-0 katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mahasimu, Simba SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wakiwemo wafungaji wa mabao, washambuliaji Amissi Tambwe wa Burundi na Mzimbabwe Donald Ngoma.
  Nafasi ya Mbuyu Twite leo amerudi Kevin Yondan ambaye Februari 20 alikuwa anatumikia adhabu ya kadi nyekundu.
  Hawa hapa; Hiki ndicho kikosi kilichoifunga Simba 2-0 Februari 20 mwaka huu Uwanja wa Taifa

  Pluijm anataka kutumia mfumo wa kujihami zaidi dhidi ya APR yenye viungo wengi wazuri na inayocheza soka ya pasi nyingi akimtumia beki Pato Ngonyani kama kiungo wa ulinzi ili kuimarisha ngome. 
  Wengine katika safu ya ulinzi ni ambao wamekuwa wakitumika katika mechi zote, kama ilivyo kwa viungo pia.
  Kikosi kinachoanza Yanga SC ni; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Vincent Bossou, Kevin Yondan, Mwinyi Hajji Mngwali, Pato Ngonyani, Deus Kaseke, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe, Donald Ngoma na Haruna Niyonzima.
  Katika benchi Pluijm atakaa na Deo Munishi ‘Dida’, Oscar Joshua, Mbuyu Twitte, Issoufou Boubakar, Salum Telela ‘Master’, Matheo Anthony na Simon Msuva.
  APR; Oliver Kwizera, Rusheshangoga, Michael Rutanga, Eric Rwatubyaye, Abdul Emily, Bayisenge Yannick, Mukunzi Fisto, Nkinzingabo, Jihadi Bizimana, Mubumbyi Bernabe, Iranzi Jean Claude  na Patrick Sibomana. 
  Kwenye benchi wapo; Jean Claude Ndoli, Rwigema Yves, Usengimana Faustin, Nshutinamagara Ismael, Benedata Jamvier, Mugenzi Biemveni na Ntamuhanga Tumaini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PLUIJM AWAPANGIA APR ‘MIDUME’ ILIYOIFANYA VIBAYA SIMBA DAR Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top