• HABARI MPYA

  Wednesday, March 09, 2016

  SIMBA WAMUACHIA UGONGWA BOBAN HADI HACHEZI KESHO MBEYA CITY NA STAND SOKOINE

  MATOKEO NA RATIBA YA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
  Machi 8, 2016
  Yanga SC 5-0 African Sports (Saa 10:30 jioni, Taifa, Dar)
  Leo; Machi 9, 2016
  Prisons Vs Kagera Sugar (Saa 10:30 jioni, Sokoine, Mbeya)
  Coastal Union Vs Mgambo JKT (Saa 10:30 jioni, Mkwakwani, Tanga)
  Mwadui FC Vs Majimaji (Saa 10:30 jioni, Mwadui, Shinyanga)
  JKT Ruvu Vs Toto Africans (Saa 10:30 jioni, Mabatini, Mlandizi)
  Kesho; Machi 10, 2016
  Simba SC Vs Ndanda FC (Saa 10:30 jioni, Taifa, Dar)
  Mbeya City Vs Stand United (Saa 10:30 jioni, Sokoine, Mbeya)
  Na Doreen Favel, MBEYA
  MBEYA City iliyo katika harakati za kujinusuru kushuka daraja, itamkosa kiungo wake 'Mtu mzima Dawa', Haruna Moshi 'Boban' (pichani kushoto) katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Stand United kesho Uwanja wa Sokoine mjini hapa.
  Boban atalazimika kusubiri mpaka Machi 14 kuingia tena kwenye kikosi cha City kufuatia kusumbuliwa na ugonjwa wa Maralia.
  Mkuu wa kitengo cha utabibu Mbeya City, Dk Joshua Kaseko ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE kwamba Boban alianza kusumbuliwa na Malaria baada ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Simba Jumapili.
  “Ni wazi hatakuwa sehemua ya mchezo kesho, ana Maralia tumekwishamtaarifu mwalimu (Kinnah Phiri) juu ya hili na tayari ameanza kufanya mazoezi maalumu na yule atakayechukua nafasi yake, imani yangu kubwa kuwa atakuwa sehemu ya kikosi march 14 wakati tutakapokuwa tunacheza na Africans Sports jijini Tanga" alisema Dk. Kaseko.
  Kaseko amesema pia kiungo mwingine wa kati, Kenny Ally Mwambungu ataukosa mchezo wa kesho kutokana na kuwa anatumikia adhabu ya kadi tatu za jano mfululizo, wakati beki Deo Julius ataendelea kuwa nje kwa maumivu ya goti.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA WAMUACHIA UGONGWA BOBAN HADI HACHEZI KESHO MBEYA CITY NA STAND SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top