• HABARI MPYA

  Wednesday, March 02, 2016

  MALINZI AANZA 'KUJIPENDEKEZA' KWA RAIS MPYA FIFA, AMTUMIA BARUA AKIMUAMBIA; "HONGERA MZEE"

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa Gianni Infantino kwa kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) mwishoni mwa wiki nchini Uswisi.
  Katika barua hiyo, ambayo BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE imepata nakala yake, Malinzi amesema TFF ina imani na ahadi zake za kuendeleza mpira wa miguu, na kwa niaba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), ataendelea kushirikiana naye katika kila jambo katika nafasi yake hiyo na kumtakia kila la kheri na mafanikiko mema.
  Malinzi akiwa na  Gianni Infantino baada ya uchaguzi wa FIFA mwishoni mwa wiki nchini Uswisi

  Wakati huo huo: Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Wanawake ya Zimbabwe, inatarajiwa kuwasili kesho Alhamis mchana wakiwa na msafara wa watu 29, wakiwemo wachezaji 20 pamoja na viongozi 9 tayari kwa ajili ya mchezo wa siku ya Ijumaa dhidi ya wenyeji Twiga Stars uwanja wa Azam Complex Chamazi.
  Zimbabwe watafikia hoteli ya DeMag iliyopo Kinondoni, ambapo jioni watapata fursa ya kufanya mazoezi katika uwanaja wa Azam Complex utakaotumika kwa mchezo siku ya Ijumaa.
  Upande wa waamuzi wa mchezo huo wanatrajiwa kuwasili kesho mchana kwa shirikia la ndege la Kenya (KQ) wakitokea nchini Ethiopia, huku kamisaa wa mchezo kutoka Congo DR akiwasili jioni kwa KQ.
  Maandalizi yote ya mchezo huo yamekamilika ambapo ulinzi na usalama utakuwepo wa kutosha, tiketi za mchezo huo zitauzwa eneo la uwanja Chamazi siku ya Ijumaa. Viingilio vya mchezo ni shilingi elfu mbili (2,000) kwa mzunguko na shilingi elfu tatu (3,000) kwa jukwaa kuu.
  TFF inawaomba wadau, wapenzi wa mpira wa miguu kujitokeza kwa wingi siku ya Ijumaa kuwapa sapoti Twiga Stars katika mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake zitakazofanyika mwishoni mwa mwaka huu nchini Cameroon.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MALINZI AANZA 'KUJIPENDEKEZA' KWA RAIS MPYA FIFA, AMTUMIA BARUA AKIMUAMBIA; "HONGERA MZEE" Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top