• HABARI MPYA

  Wednesday, March 02, 2016

  APR YAMPA MWARABU JUKUMU LA KUIFUTA YANGA LIGI YA MABINGWA

  TIMU ya jeshi la Rwanda, APR inatarajiwa kuingia Mkataba na kocha Nizar Khanfir, raia wa Tunisia ili achukue nafasi ya Mserbia Ljupko Petrovic (pichani kushoto), aliyeondoka mwishoni mwa mwaka jana.
  APR imekuwa chini ya kocha wa akademi yake, Emmanuel Rubona tangu kuondoka kwa Petrovic na Msaidizi wake, Mserbia mwenzake, Dusan Dule wakihamia PFC Litex Lovech ya Bulgaria na sasa Khanfir anatarajiwa kusaini Mkataba na kuwa Mwarabu wa kwanza kufundisha Rwanda.
  Na hatua ya kumchukua kocha huyo wa zamani wa timu ya Stade Gabesien ya Tunisia, inakuja baada ya APR kuingia Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ambako itakutana na Yanga SC.
  Na mwalimu huyo mpya anatarajiwa kutua Kigali wakati wowote na atatambulishwa rasmi Jumapili.
  Machi 11 APR watakuwa wenyeji wa Yanga katika mchezo wa kwanza Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika, kabla ya timu hizo kurudiana wiki moja baadaye Dar es Salaam. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: APR YAMPA MWARABU JUKUMU LA KUIFUTA YANGA LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top