• HABARI MPYA

  Tuesday, March 08, 2016

  REAL MADRID YA ZIDANE YASAKA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA LEO

  RATIBA LIGI YA MABINGWA ULAYA
  Leo Machi 8, 2016
  Real Madrid Vs Roma (Saa 4:45 usiku, Santiago Bernabeu)
  VfL Wolfsburg Vs KAA Gent (Saa 4:45 usiku, Volkswagen Arena)
  Kesho Machi 9, 2016
  Zenit St Petersburg Vs Benfica (Saa 2:00 usiku, Petrovski)
  Chelsea Vs Paris Saint-Germain (Saa 4:45 usiku, Stamford Bridge)
  Kocha wa Real Madrid, Zinadine Zidane anaiongoza timu yake katika hatua muhimu leo Ligi ya Mabingwa Ulaya

  MABINGWA wa kihistoria Ulaya, Real Madird usiku wa leo wanaikaribisha AS Roma Uwanja wa Santiago Bernabeu katika mchezo wa marudianio wa hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa.
  Real wanatarajiwa kuwa na kazi nyepesi tu leo nyumbani, baada ya ushindi wa 2-0 kwenye mchezo wa kwanza Februari 17, Uwanja wa Olimpiki mjini Roma, mabao ya Cristiano Ronaldo na Jese Rodriguez.
  Mchezo mwingine wa Ligi ya Mabingwa leo ni kati ya VfL Wolfsburg watakaokuwa wenyeji wa KAA Gent Uwanja wa Volkswagen. Ikumbukwe mchezo wa kwanza, Wolfsburg ilishInda 3-2 ugenini.
  Michuano hiyo itaendelea kesho, Chelsea wakiikaribisha Paris Saint-Germain Uwanja wa Stamford Bridge, London.
  Chelsea itahitaji ushindi mwembamba tu, baada ya awali kufungwa mabao 2-1 mjini Paris. 
  Mchezo mwingine wa kesho ni kati ya Zenit St Petersburg dhidi ya Benfica Uwanja wa Petrovski. Ikumbukwe mchezo wa kwanza, Benfica ilishinda 1-0 nyumbani Ureno.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REAL MADRID YA ZIDANE YASAKA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA LEO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top