• HABARI MPYA

  Wednesday, March 09, 2016

  COASTAL YAILAZA MGAMBO 1-0 MKWAKWANI, JKT RUVU NAYO YAIPIGA 2-1 TOTO MLANDIZI

  BAO pekee la mshambuliaji Ally Ahmed ‘Shiboli’ leo limeipa ushindi wa 1-0 Coastal Union dhidi ya ndugu zao, Mgambo JKT katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
  Ushindi huo, unaifanya Coastal inayofundishwa na mchezaji wake wa zamani, Ally Jangalu ifikishe pointi 19 baada ya kucheza mechi 22 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 14, kutoka mkiani.

  Mgambo JKT inabaki na pointi zake 19 baada ya kucheza mechi 22 na kuendelea kushika nafasi ya 13, ikiizidi kwa wastani mabao Coastal.  
  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Mwadui FC imelazimishwa sare ya bila kufungana na Majimaji ya Songea Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga, Prisons imetoka sare ya 1-1 na Kagera Sugar Uwanja wa Sokoine, Mbeya na JKT Ruvu imeifunga 2-1 Toto Africans Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: COASTAL YAILAZA MGAMBO 1-0 MKWAKWANI, JKT RUVU NAYO YAIPIGA 2-1 TOTO MLANDIZI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top