• HABARI MPYA

  Thursday, March 10, 2016

  CHELSEA YAAGA 'KIBWEGE' LIGI YA MABINGWA, YAPIGWA NJE NDANI NA PSG

  Mshambuliaji wa PSG ya Ufaransa, Zlatan Ibrahimovic akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao la ushindi ikiilaza Chelsea 2-1 usiku wa Jumatano Uwanja wa Stamford Bridge na kutinga Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa ushindi wa jumla wa 4-2, baada ya awali kushinda pia 2-1 mjini Paris. Bao lingine la PSG limefungwa na Adrien Rabiot, wakati la Chelsea limefungwa na Diego Coasta PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Kipa wa Benfica, Ederson akimzuia mshambuliaji wa Zenit Petersburg, Artem Dzyuba kufunga katika mchezo wa marudiano wa hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumatano Uwanja wa Petrovskij mjini St. Petersburg. Benfica ilishinda 2-1, mabao yake yakifungwa na Nicolas Gaitan na Talisca, baada ya Hulk kutangulia kuwafungia wenyeji. Benfica inaungana na PSG na Real Madrid kutangulia Robo Fainali kwa ushindi wa jumla wa 3-1, baada ya awali kushinda 1-0 Ureno PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YAAGA 'KIBWEGE' LIGI YA MABINGWA, YAPIGWA NJE NDANI NA PSG Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top