• HABARI MPYA

  Saturday, March 12, 2016

  BURKINA FASO YAMUITA KIPA WA GHANA KUIZUIA UGANDA AFCON

  KIPA wa Hearts of Oak ya Ghana, Soulama Abdoulaye ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Burkina Faso kwa ajili ya mchezo dhidi ya Uganda  kufuzu Fainali za Mataifa ta Afrika.
  Kutakuwa na mechi mbili za nyumbani na ugenini baina ya timu hizo katika Kundi D wiki ijayo. Kocha wa Stallions, Paulo Duarte ametaja kikosi cha wachezaji 25, ambacho ndani yake amemjumuisha kipa mzoefu anayecheza ligi ya Ghana.

  Kipa wa Hearts of Oak ya Ghana, Soulama Abdoulaye ameijumuishwa kikosi cha Burkina Faso kitakachoivaa Uganda

  Soulama amekuwa chaguo la kwanza kwa muda mrefu, lakini alikuwa benchi katika mchezo uliopita wa kufuzu dhidi ya Bostwana, Burkina ikifungwa 1-0, jambo ambalo lilisababisha kocha huyo Mreno alaumiwe kwa kumuweka benchi Abdoulaye.
  Kikosi  cha Duarte kinashika nafasi ya tatu Kundi D wakati Uganda inaongoza msimamo wa kundi hilo kwa pointi zake sita. 
  Burkina Faso imedhamiria kusimamisha wimbi la ushindi la The Cranes. Mchezo wa kwanza utafanyika mjini Ouagadougou Machi 26, wakati marudiano yatakuwa Kampala siku tatu baadaye.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BURKINA FASO YAMUITA KIPA WA GHANA KUIZUIA UGANDA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top