• HABARI MPYA

  Monday, March 11, 2019

  BIASHARA UNITED YANG’ARA NYUMBANI MUSOMA, YAICHAPA NDANDA FC 2-0 LIGI KUU LEO

  TIMU ya Biashara United ya Mara leo imeutumia vyema Uwanja wa nyumbani, Karume mjini Musoma mkoani Mara kwa kuichapa Ndanda FC mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
  Ushindi huo wa Biashara United leo umetokana na mabao ya wachezaji wake tegemeo, Tariq Kiakala dakika ya 51 na George Makang’a dakika ya 58 
  Na kwa ushindi huo, Biashara United inayofundishwa na kocha Amri Said ‘Stam’ inafikisha pointi 27 baada ya kucheza mechi 28, ingawa inabaki nafasi ya 19 mbele ya African Lyon inayoshika mkia kwa pointi zake 22 za mechi 30 na nyuma ya Ndanda hiyo hiyo inayobaki na pointi zake 33 za mechi 28 pia. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BIASHARA UNITED YANG’ARA NYUMBANI MUSOMA, YAICHAPA NDANDA FC 2-0 LIGI KUU LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top