• HABARI MPYA

  Sunday, March 10, 2019

  ARSENAL YAZIMA REKODI YA SOLSKJAER KUTOFUNGWA MAN UTD

  Pierre-Emerick Aubameyang akishangilia baada ya kuifungia Arsenal bao la pili kwa penalti dakika ya 69 baada ya Fred kumuangusha Alexandre Lacazette kwenye boksi katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Manchester United leo kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Emirates mjini London na kumaliza rekodi ya kocha ya kocha mpya, Ole Gunnar Solskjaer kutofungwa kwenye ligi hiyo tangu achukue nafasi ya Jose Mourinho aliyefukuzwa. Bao la kwanza la Arsenal limefungwa na kufuatia Granit Xhaka dakika ya 12 na kwa ushindi huo, Washika Bunduki wa London wanarejea nafasi ya nne wakifikisha pointi 60 baada ya kucheza mechi 30, sasa wakiizidi kwa pointi mbili Manchester United inayorudi nafasi ya tano ikiizidi pointi moja tu Chelsea iliyocheza mechi 29 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAZIMA REKODI YA SOLSKJAER KUTOFUNGWA MAN UTD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top