• HABARI MPYA

    Sunday, January 21, 2018

    TAYARI SANCHEZ NI MCHEZAJI WA MAN UNITED, MKHITARYAN ARSENAL

    MSHAMBULIAJI Alexis Sanchez amewasili Manchester kwa ajili ya kufanyiwa vipimko vya afya makao makuu ya klabu viwania vya Carrington leo ili kukamilisha uhamisho wa kubadilishana wachezaji kutoka Arsenal.
    Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ameweka wazi kwa kusema; "Nafikiri tunaelekea kufanikiwa,".
    Kiungo wa United, Henrikh Mkhitaryan amefikia makubaliano ya vipengele binafsi na Arsenal, lakini pia The Gunners wameanza mazungumzo ya kumununua kwa Pauni Milioni 44 mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang.
    Ofa yao ya kwanza ilikataliwa, lakini wanatarajiwa kupeleka nyingine.

    Hatimaye Manchester United imekamilisha usajili wa Alexis Sanchez kutoka Arsenal PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

    Pamoja na hayo, Mourinho alisema baada ya mechi na Burnley, United wakishinda 1-0 kwamba alijua mwishowe atampata mchezaji huyo. 
    Sanchez, mwenye umri wa miaka 29, ataingiza kiasi cha Pauni 450,000 kwa wiki katika mkataba wa miaka minne na nusu Old Trafford baada ya United kubomoa benki kuwapiku mahasimu wake, Manchester City na Chelsea.
    Leo Sanchez alitarajiwa kuwasili mapema Carrington kati ya Saa 7:00 mchana na Saa 9:00 Alasiri wakati wachezaji wenzake wapya wamepewa siku mbili za mapumziko kuelekea mechi ya Kombe la FA ijumaa dhidi ya Yeovil na Jose Mourinho amesafiri kwenda London kukaa na familia yake nyumbani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TAYARI SANCHEZ NI MCHEZAJI WA MAN UNITED, MKHITARYAN ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top