• HABARI MPYA

  Thursday, January 18, 2018

  SANCHEZ AONDOLEWA MAZOEZINI KIKOSI CHA KWANZA ARSENAL

  Alexis Sanchez akionyesha ishara ya dole kuashiria mambo safi wakati anaondoka viwanja vya mazoezi vya Arsenal leo mchana PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  WACHEZAJI 10 WANAOLIPWA ZAIDI MAN UNITED

  1. Alexis Sanchez - Pauni 450,000 kwa wiki
  2. Paul Pogba - Pauni 260,000 kwa wiki
  3. Romelu Lukaku - Pauni 220,000 kwa wiki
  4. David de Gea - Pauni 200,000 kwa wiki
  5. Zlatan Ibrahimovic - Pauni 150,000 kwa wiki
  6. Juan Mata - Pauni 145,000 kwa wiki
  7. Nemanja Matic - Pauni 140,000 kwa wiki
  = Henrikh Mkhitaryan - Pauni 140,000 kwa wiki
  9. Marouane Fellaini - Pauni 120,000 kwa wiki
  10. Chris Smalling - Pauni 120,000 kwa wiki
  HARAKATI za Alexis Sanchez kuhamia Manchester United zimechukua sura mpya baada ya Mchile huyo kuondolewa kwenye mazoezi ya kikosi cha kwanza cha Arsenal.
  Mchile huyo anajiandaa kujiunga na United katika dili ambalo litafanya kiungo Henrikh Mkhitaryan ahamie upande wa pili.
  Sanchez aliwasili viwanja vya mazoezi vya Arsenal, Colney mjini London kwa ajili ya mazoezi, lakini akaenda kufanya mazoezi na timu ya watoto kuelekea mechi ya Jumamosi dhidi ya Crystal Palace.
  Kufanya mazoezi na timu ya watoto moja kwa moja kunaonyesha kwamba mpango wa Sanchez kuhamia Old Trafford unakaribia kukamilika.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amekubali malipo ya Pauni 450,000 kwa wiki Man United, kati ya hizo Pauni 350,000 ni mshahara na Pauni 100,000 ni malipo ya hakinza picha zake, wakati pia atalipwa ada ya kusaini Pauni Milioni 7.5 kwa mwaka katika miaka minne. 
  Mapema leo, kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kwamba dili hilo linaweza kukamilika ndani ya saa 48 na akasema ikiwa uhamisho huo hautakamilika, Sanchez atajumuishwa kwenye kikosi kitakachoivaa Eagles.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SANCHEZ AONDOLEWA MAZOEZINI KIKOSI CHA KWANZA ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top