• HABARI MPYA

  Saturday, January 20, 2018

  NYIGU WA RWANDA WAING'ATA EQUATORIAL GUINEA 1-0 CHAN

  MICHUANO ya CHAN imeendelea jana kwa mechi mbili za Kundi C, watoto Paul Kagame, Nyigu wa Rwanda wakiwang’ata Equatorial Guinea 1-0, bao pekee la Thierry Manzi dakika ya 66 Uwanja wa Ibn Batouta mjini Tanger, Morocco.
  Mechi iliyotangulia Nigeria waliwachapa Libya 1-0 bao pekee la Sunday Faleye dakika ya 79 hapo hapo Ibn Batouta.
  Matokeo hayo yanamaanisha Rwanda wanaungana na Nigeria kuongoza Kundi C baada ya kila timu kufikisha pointi nne, kufuatia awali katika mechi baina yao kutoka sare ya 0-0.
  Libya wanashika nafasi ya tatu kwa pointi zao tatu walizovuna kwa ushindi dhidi ya Equatorial Guinea wanaoshika mkia wakiwa hawana pointi.
  Habari mbaya kwa wana CECAFA ni Uganda kupoteza mechi ya pili mfululizo juzi baada ya kufungwa 1-0 na Namibia bao pekee la Panduleni Nekundi dakika ya 90 ]katika mchezo wa Kundi B  Uwanja wa Marrakech.
  The Cranes  inayofundishwa na kocha Mfaransa,  Sebastien Desabre tangu D baada esemba mwaka jana sasa imeaga mashindano ya kufungwa 3-1 na Zambia katika mchezo wa kwanza Januari 14.
  Kwa ushindi wake, Namibia inaungana na Zambia iliyoshinda 2-0 dhidi ya Ivory Coast juzi, mabao ya Augustine Mulenga dakika za nane na 73 hapo hapo Uwanja wa Marrakech kwenda Robo Fainali.
  Ikumbukwe kutoka Kundi A tayari Morocco na Sudan zimefuzu Robo Fainali na michuano hiyo inaendelea leo kwa mechi za Kundi D Uwanja wa Agadir mjini Agadir, Angola wakimenyana na Cameroon kuanzia Saa 1:30 usiku na Kongo dhidi ya Burkina Faso kuanzia Saa 4:30 usiku,
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NYIGU WA RWANDA WAING'ATA EQUATORIAL GUINEA 1-0 CHAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top