• HABARI MPYA

  Friday, December 15, 2017

  BOCCO AENDELEZA MOTO WA MABAO SIMBA IKIUA 4-0 CHAMAZI

  Na Salma Suleiman, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI John Raphael Bocco ameendelea kuwa mwiba kwenye mechi za kirafiki Simba SC baada ya leo kufunga mabao mawili na kuseti moja timu hiyo ikishinda 4-0 dhidi ya African Lyon Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.  
  Bocco aliyefunga mabao mawili pia wiki iliyopita katika ushindi wa 3-1 ya timu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC  hapo hapo Chamazi, leo amefunga bao mola kila kipindi.
  Mchezaji huyo wa zamani wa Azam FC, alimtilia krosi nzuri chipukizi Moses Kitandu kutoka wingi ya kulia kuifungia Simba bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 17.
  John Bocco amefunga mabao mawili na kuseti moja Simba ikishinda 4-0 dhidi ya African Lyon leo  

  Kitandu aliyepandishwa kutoka timu ya vijana ya Simba msimu huu, naye akalipa kwa kumpasia Bocco kuifungia timu hiyo bao la pili dakika ya 28.
  Kipindi cha pili, Simba waliendelea kucheza vizuri kwa uelewano mkubwa na kufanikiwa kupata bao la tatu dakika ya 55 kupitia kwa kinda Kelvin Faru aliyemalizia pasi maridadi ya Hamisi Ndemla.
  Bocco akakamilisha shamrashamra za mabao za Wekundu wa Msimbazi kwa kufunga bao zuri la nne dakika ya pili ya muda wa nyongeza baada ya kutimia dakika 90 za kawaida.
  Kikosi cha Simba SC leo kilikuwa; Emanuel Mseja/Ally Salim dk82, Ally Shomari Ally, Paul Bukaba, Yussuf Mlipili, Juuko Murshid, Said Ndemla, Kelvin Faru, Mwinyi Kazimoto/Dadi Mbarouk dk90+3, John Bocco/Khalifa Hassan dk90+3, Jamal Mwambeleko na Moses Kitandu/Rashid Juma dk87.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BOCCO AENDELEZA MOTO WA MABAO SIMBA IKIUA 4-0 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top