• HABARI MPYA

  Sunday, October 22, 2017

  WYDAD CASABLANCA, TP MAZEMBE ZATANGULIA FAINALI MICHUANO YA AFRIKA

  MABAO mawili ya Achraf Bencharki na lingine la Walid El Karti jana yameipa ushindi wa 3-1 Wydad Casablanca dhidi ya USM Alger na kuingia fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Mohamed V mjini Casablanca usiku wa jana, bao la kufutiaa machozi la USM Algver lilifungwa na Ayoub Abdellaoui na sasa Wydad inakwenda fainali kwa ushindi wa 3-1 baada ya sare ya 0-0 kwenye mchezo wa kwanza.
  Karti alifunga dakika ya 26 na Bencharki akafunga dakika za 54 na 90 na ushei, wakati Abdellaoui aliwafungia USM Alger dakika ya 67.
  Nusu fainali nyingine ya pili ya Ligi ya Mabingwa itazikutanisha, wenyeji Al Ahly SC na  Etoile du Sahel ya Tunisia Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria, Misri kuanzia Saa 2:00 usiku leo. 
  Ahly wanahitaji hata ushindi wa 1-0 ili kwenda Fainali, baada ya kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza Oktoba 1 Uwanja wa Olimpiki mjini Sousse, Tunisia.
  Wakati huo huo: TP Mazembe imetoa sare ya 0-0 na wenyeji, FUS Rabat katika mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Afrika usiku wa jana Uwanja wa FUS mjini Rabat nchini Morocco.
  Matokeo hayo yanamaanisha Mazembe inakwenda fainali baada ya kushinda 1-0 kwenye mchezo wa kwanza nyumbani.
  Timu hiyo ya DRC, sasa itakutana na mshindi wa jumla kati ya SuperSport United ya Afrika Kusini na Club Africain ya Tunisia katika fainali mwezi ujao.
  SuperSport wamesafiri kuifuata Africain nchini Tunisia kwa mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya michuano hiyo leo, wakitoka kutoa sare ya 1-1 Oktoba 1 mjini Pretoria.
  Kikosi cha Wydad Casablanca kilikuwa: Laaroubi, Rabeh, Noussir, Atouchi, Saidi, Karti, Nakach, Gaddarine/Hachimi dk64, Bencharki, Ounajem/Aoulad dk85 na Haddad/Khadrouf dk74.
  USM Alger: Zemmamouche, Meftah, Benmoussa, Chafaï, Abdellaoui, Sayoud, Benkhemassa, Benguit/Hamzaoui dk69, Yaya/Beldjilali dk75, Meziane na Darfalou.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WYDAD CASABLANCA, TP MAZEMBE ZATANGULIA FAINALI MICHUANO YA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top