• HABARI MPYA

  Tuesday, October 17, 2017

  WATANO KUKIONGEZEA NGUVU KIKOSI CHA YANGA TABORA LEO

  Na Adam Hhando, TABORA
  WACHEZAJI watano kati ya nane waliobaki Dar es Salaam wakati kikosi cha Yanga kinakwenda Kanda ya Ziwa kwa mechi zake za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wanatarajiwa kuungana na timu hiyo mjini Tabora leo.
  Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online mjini hapa leo kwamba wachezaji hao ni kipa Ramadhan Kabwili, mabeki Pato Ngonyani, Abdallah Hajji ‘Ninja’ na viungo Juma Mahadhi na Saidi Mussa.
  Saleh amesema kwamba wachezaji watatu, kiungo Thabani Kamusoko na washambuliaji Mzimbabwe mwenzake, Donald Ngoma na Mrundi Amissi Tambwe watabaki Dar es Salaam kuendelea na matibabu.
  Juma Mahadhi (kushoto) akipambana na kiungo wa Simba, Mghana James Kotei Agosti 23, mwaka huu

  Saleh amesema kwamba wachezaji hao wanatarajiwa kuungana na timu itakaporejea Dar es Salaam wiki ijayo baada ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Stand United Jumapili wiki hii mjini Shinyanga.
  Inaonekana wachezaji hao wamepewa mapumziko zaidi kwa makusudi zaidi ili wawe fiti zaidi kwa ajili ya mchezo dhidi ya mahasimu wa jadi, Simba Oktoba 28, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.   
  Yanga ipo mjini Tabora tangu juzi usiku kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Rhino Rangers inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza ambao utafanyika kesho Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
  Baada ya mchezo huo, itaendelea na mazoezi kabla ya Ijumaa kwenda Shinyanga ambako watakuwa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya wenyeji, Stand United.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WATANO KUKIONGEZEA NGUVU KIKOSI CHA YANGA TABORA LEO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top