• HABARI MPYA

  Tuesday, October 17, 2017

  OVERMARS AREJEA ARSENAL KUMSAIDIA WENGER KUSAJILI

  MWANASOKA wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa, Marc Overmars anatarajiwa kurejea Arsenal kama Mkurugenzi wa Soka kuanzia msimu ujao.
  Winga huyo wa zamani wa Washika Bunduki hao, ambaye alicheza mechi 141 na kufunga mabao 40 kuanzia mwaka 1997 na mwaka 2000, amekuwa Mkurugenzi wa Soka wa Ajax tangu mwaka 2012, lakini anatarajiwa kurudi London.
  Overmars, mwenye umri wa miaka 44, anatarajiwa kuchukua majukumu mengi yaliyokuwa yanafanywa na Dick Law, aliyekuwa anashughulia mausala ya usajili ya klabu kabla ya kuondoka mwishoni mwa msimu uliopita.
  Kocha Arsene Wenger wakati wote amekuwa akisita kufanya kazi kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Soka na mapema mwaka huu, alismea: "Sijawahi kuelewa inamaanisha nini, Mkurugenzi wa Soka. Mimi ni kocha wa Arsenal na nikiwa kocha, nitaamua nini cha kufanya kwenye masuala ya kiufundi. Ni hivyo,".

  Marc Overmars anatarajiwa kurejea Arsenal msimu ujao kama Mkurugenzi wa Soka PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  Pamoja na yote, bado Overmars ni mtu muhimu kujiunga na timu kutokana na uzoefu wake wa miaka mitano kwenye masuala ya kiufundi alipokuwa na Ajax nchini Uholanzi.
  Nyuma ya pazia, mtikisiko ulitokea baada ya klabu kushindwa kuwasajili wachezaji iliyowataka wakiwemo nyota wawili wa Monaco, Kylian Mbappe na Thomas Lemar, licha ya kuweka ofa ya Pauni Milioni 92.
  Pia walishindwa kuwapata Julian Draxler wa PSG katika siku ya mwisho ya kufunga ya pazia la usajili ili waweze kumuuza kwa Pauni Milioni 60 mshambuliaji wao, Alexis Sanchez kwenda Manchester City.
  Arsenal ilifungwa 2-1 na Watford kwenye mchezo wake uliopita wa Ligi Kuu ya England na Alhamisi itashuka tena dimbani kumenyana na Red Star Belgrade kwenye michuano ya Europa League.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: OVERMARS AREJEA ARSENAL KUMSAIDIA WENGER KUSAJILI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top