• HABARI MPYA

  Friday, October 13, 2017

  SAMATTA AKOSA PENALTI MBEYA CITY YATOA SARE 2-2 NA MBAO KIRUMBA

  Na Mwandishi Wetu, MWANZA
  TIMU ya Mbao FC imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
  Mbao watajilaumu wenyewe kwa sare hiyo, kwani waliuanza mchezo vizuri na kuwatangulia wageni wao kwa mabao 2-0 hadi mapumziko.
  Mabao hayo yalifungwa na Nahodha wake, Mrundi Yussuf Ndikumana aliyefunga kwa shuti la mpira wa adhabu dakika tatu na Ndaki Robert dakika ya 41.
  Mbeya City wakazinduka na wakaanza kwa Mohammed Samatta kukosa penalti kufuatia Ndikumana kucheza rafu.
  Lakini kipindi cha pili Mbeya City wakasawazisha kupitisa Eliud Ambokile dakika ya 55 na Omar Ramadhani dakika ya 63.
  Mohammed Samatta (katikati) leo amekosa penalti dhidi ya Mbao FC mjini Mwanza

  Ligi Kuu inatarajiwa kuendelea kesho na mabingwa hao watetezi, Yanga wakiwa wageni wa Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Mwadui FC wakiikaribisha Azam FC Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga na Ndanda wakiwakaribisha jirani zao, Maji Maji ya Songea Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara wakati Singida United itasafiri hadi Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi kucheza na wenyeji Ruvu Shooting ya Pwani.
  Majirani wengine, Njombe Mji na Lipuli ya Iringa watacheza kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe ilihali michezo mingine ya Ligi hiyo ikifanyika Jumapili Oktoba 15, ambako Simba itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam wakati Tanzania Prisons itacheza na Stand United kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA AKOSA PENALTI MBEYA CITY YATOA SARE 2-2 NA MBAO KIRUMBA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top