• HABARI MPYA

    Thursday, October 12, 2017

    SAINTFIET AULA ULAYA, LAKINI ASEMA; “NAWAKUMBUKA SANA YANGA”

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    KOCHA wa Mbelgiji, Tom Saintfiet amesaini mkataba wa miaka miwili kufundisha timu ya taifa ya Malta, lakini amesema bado anaikumbuka Yanga, timu yake ya zamani.
    “Oooh Yanga, siwezi kuwasahau, bado ni mabingwa huko? Nawakumbuka sana,”alisema Saintfiet akizungumza kwa simu na Bin Zubeiry Sports – Online jana.
    Mbelgiji huyo amesema kwamba anajivunia kukubali mkataba wa miaka miwili kufundisha timu yake ya kwanza ya taifa barani Ulaya, Malta. 
    “Nina furaha sana kupata kazi ya kufundisha timu ya kwanza ya taifa ya Ulaya na kwa hakika timu hii ni chaguo zuri kwangu. “Baada ya miakataba ya muda mfupi mfupi, ni vizuri kufanya Malta miaka ijayo na kujaribu kuinua soka yao,” alisema.
    Tom Saintfiet (kulia) amesema bado anaikumbuka sana Yanga, timu yake ya zamani

    Tom Saintfiet aliyezaliwa Machi 29, mwaka 1973 mjini Mol, Ubelgiji ni kocha mwenye leseni ya UEFA PRO na awali alicheza soka kuanzia mwaka 1983 hadi 1997 katika klabu za FC Boom, K.V.C. Westerlo, K.F.C. Lommel S.K. na K.F.C. Verbroedering Geel.
    Alianza ukocha akiwa ana umri wa miaka 24 tu, akiweka rekodi ya kocha kijana zaidi katika soka ya Ubelgiji akianza na timu za madfaraja ya chini kuanzia mwaka 197 hadi 2001, kabla ya kuhamia Satelitte Abidjan ya Ivory Coast alikodumu hadi 2002 alipokwenda B71 Sandur.
    Amefundisha pia Stormvogels Telstar, Al-Gharafa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Qatar, BV Cloppenburg, FC Emmen alipokuwa Mkurugenzi wa Ufundi, RoPS, Namibia, Zimbabwe, Shabab Al-Ordon, Ethiopia kabla ya kuja Yanga SC mwaka 2012 ambako alidumu kwa miezi mitatu kabla ya kwenda Yemen, baadaye Malawi, klabu ya Free State Stars ya Afrika Kusini, Togo na Bangladesh mwaka jana.
    Desemba 7 mwaka jana aliteuliwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Trinidad & Tobago ambako alijiuzulu baada ya mechi nne tu Januari 10, mwaka huu na sasa anakwenda kuanza maisha mapya Malta.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAINTFIET AULA ULAYA, LAKINI ASEMA; “NAWAKUMBUKA SANA YANGA” Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top