• HABARI MPYA

  Thursday, October 12, 2017

  AHMED MUSA AFUNGUA KITUO CHA KUUZIA MAFUTA NIGERIA

  SI jambo geni kwa wanasoka kujikita kwenye biashara duniani katika kujiandaa na maisha yao ya baadaye wakistaafu.
  Na mshambuliaji wa Leicester City, Ahmed Musa mapema tu naye anaanza kujiandalia maisha yake ya baadaye kwa kufungua biashara.
  Nyota huyo wa Nigeria ana umri wa miaka 24, lakini amefungua kituo cha kuuzia mafuta mjini Kano, kilomita 500 Kaskazini mwa nyumbani kwao, Jos.
  Musa alirejea nyumbani kwa mechi za kufuzu Kombe la Dunia, lakini akatumia muda huo huo kufungua kituo cha kuuzia mafuta na akashiriki mwenyewe kuwajazia mafuta wateja waliojitokeza katika siku ya uzinduzi wa kituo hicho.
  Ahmed Musa akimuwekea mteja mafuta kwenye gari wakati wa uzinduzi wa kituo chake cha mafuta PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Na huu si mradi wa kwanza wa Musa, kwani tayari ana biashara nyingine kama zikiwemo mali zisizohamishika na vituo vya Michezo na Mazoezi.
  Licha ya eneo hilo kuwa ni umbali wa saa tano kwa kuendesha gari kutoka sehemu aliyozaliwa, Musa anafahamika mno huko kwa sababu ndiko alipoanzia soka yake akiwa na klabu ya Pillars.
  Kutoka hapo, akaenda VVV-Venlo nchini Holland, kabla ya kuhamia CSKA Moscow ya Urusi na sasa Leicester. Alipokuwa CSKA Moscow alikutana na Nahodha wa Tanzania, Mbwana Samatta ambaye kufanya majaribio timu hiyo na kufuzu, lakini klabu yake ya zamani TP Mazembe iligoma kumuuza.
  Kwa sasa Samatta anachezea KRC Genk ya Ubelgiji ambako Mazembe ilimuuza Januari mwaka jana. 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AHMED MUSA AFUNGUA KITUO CHA KUUZIA MAFUTA NIGERIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top