• HABARI MPYA

  Friday, October 13, 2017

  KANTE NJE WIKI TATU CHELSEA BAADA YA KUUMIA UFARANSA

  KOCHA wa Chelsea, Antonio Conte amesema kiungo Mfaransa, N'Golo Kante atakuwa nje ya Uwanja kwa wiki tatu baada ya kuumia nyama za paja kwenye timu yake ya taifa.
  Kante alilazimika kutoka nje anachechemea kipindi cha kwanza katika mchezo wa Ufaransa wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Bulgaria mwishoni mwa wiki iliyopita na Conte anataraji mchezaji huyo atakuwa nje kwa mwezi wote wa Oktoba.
  "Kante ataenda kufanyiwa vipimo vingine wiki ijayo kuangalia kama hali yake inaendelea vizuri. Kutokana na vipimo vya awali, labda atakuwa nje kwa siku 20 au 21," amesema Conte leo.
  N'Golo Kante atakuwa nje ya Uwanja kwa wiki tatu baada ya kuumia nyama za paja kwenye timu yake ya taifa

  Kante, mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa PFA msimu uliopita, ataukosa mchezo wa kesho wa Chelsea dhidi ya wenyeji, Crystal Palace na anaweza kukosekana kwenye mechi nyingine zote mwezi huu.
  Hizo ni pamoja na mbili za Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Roma, mechi za Ligi Kuu ya England dhidi ya Watford na Bournemouth na ya Kombe la Ligi dhidi ya Everton.
  Conte amesema kukosekana kwa Kante kunaichia pigo timu yake, Chelsea ikiwa katika kipindi kigumu hususan baada ya kiungo wa England, Danny Drinkwater, aliyesajiliwa kutoka Leicester mwezi Agosti pia kuwa nje kwa sababu ya maumivu.
  Chelsea, wanaoshika nafasi ya nne wana pointi sita nyuma ya Manchester City, baada ya mabingwa hao watetezi kufungwa 1-0 na vinara hao wa Ligi Kuu kwenye mchezo uliopita kabla ya kwenda kwenye mapumziko ya kupisha mechi za kufuzu Kombe la Dunia.
  Conte ni ongezeko la majeruhi ndani ya Chelsea, baada ya mshambuliaji wa Hispania, Alvaro Morata ambaye naye atakosa mechi dhidi ya Palace kwa sababu ya maumivu ya nyama za paja.
  Morata hakuichezea Hispania mwishoni mwa wiki, lakini Conte anatumai atarejea kuivaa Roma Uwanja wa Stamford Bridge Jumatano.
  "Natumai kumpata tena Morata haraka sana, natumai kwa mchezo ujao,"amesema Conte.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KANTE NJE WIKI TATU CHELSEA BAADA YA KUUMIA UFARANSA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top