• HABARI MPYA

  Wednesday, October 04, 2017

  NDEMLA AFUNGA ‘BAO LA AJABU’ SIMBA SC YAICHAPA 1-0 DODOMA FC

  Na Rehema Lucas, DODOMA
  BAO pekee la kiungo Said Hamisi Ndemla jioni ya leo limetosha kuipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Dodoma FC katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
  Ndemla alifunga bao hilo dakika ya 72 kwa shuti la umbali wa mita 40 baada ya kumchungulia kipa Jackson Chove aliyekuwa amezubaa langoni mwake. 
  Said Ndemla amefunga bao pekee leo Simba SC imeshinda 1-0 dhidi ya wenyeji, Dodoma FC Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma


  Pamoja na kufungwa, Dodoma FC inayofundishwa na kocha na mchezaji wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ilicheza vizuri na haikuwa na bahati ya kufunga tu.
  Kwa Simba ya kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog mchezo huu ulikuwa ni maandalizi ya mchezo wake ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar, wakati Dodoma nayo inajiandaa na mechi zake za Daraja la Kwanza.  
  Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Emmanuel Mseja, Ally Shomary, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Yussuf Mlipili, Juuko Murshid, Jonas Mkude, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim, Said Ndemla, Laudit Mavugo, Juma Liuzio na Jamal Mnyate.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NDEMLA AFUNGA ‘BAO LA AJABU’ SIMBA SC YAICHAPA 1-0 DODOMA FC Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top