• HABARI MPYA

    Monday, October 09, 2017

    MTIHANI WA KUPANDISHA MAREFA KUFANYIKA OKTOBA 12 HADI 15, DAR NA MWANZA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MTIHANI wa mazoezi ya utimamu wa mwili kwa waamuzi wa Daraja la Tatu na Pili kuwania kupanda unatarajiwa kufanyika Oktoba 12 hadi 15, mwaka huu katika vituo viwili Dar es Salaam na Mwanza.
    Zoezi hilo litajumuisha pia wale waamuzi wa Daraja la Kwanza walioshindwa mitihani hiyo mwezi Agosti, mwaka huu. Hivyo nao wanaruhusiwa kwenda kufanya mitihani tena.
    Kituo cha Dar es Salaam kitakuwa na waamuzi wa mikoa ya Dar es Salaam yenyewe, Pwani, Morogoro, Tanga, Kilimanjaro, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Njombe, Iringa, Mbeya, Rukwa na Songwe.
    Kituo cha Mwanza kitakuwa na waamuzi wa mikoa ya Mwanza yenyewe, Mara, Kagera, Simiyu, Geita, Kigoma, Arusha, Shinyanga, Tabora, Dodoma, Singida, Manyara na Katavi.
    Waamuzi wote waende kwenye vituo vyao walivyopangiwa kama ilivyoelekezwa Oktoba 12, 2017 - ni siku ya kupima afya kabla ya kuanza kwa mitihani mingine ukiwamo wa utimamu wa mwili.
    Wakati huo huo: Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amempongeza Juliana Shonza kwa kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. John Pombe Magufuli mwishoni mwa wiki akichukua nafasi ya Anastazia Wambura.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MTIHANI WA KUPANDISHA MAREFA KUFANYIKA OKTOBA 12 HADI 15, DAR NA MWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top