• HABARI MPYA

  Thursday, October 12, 2017

  FALCAO ADAIWA KUWARUBUNI WACHEZAJI PERU WAPANGE MATOKEO

  MSHAMBULIAJI wa Colombia, Radamel Falcao ameingia lawamani akituhumiwa kuwaambia wachezaji wa timu pinzani wacheze pole pole ili watoe nao sare katika mechi ya mwisho ya kufuzu Kombe la Dunia 2018 Urusi
  Colombia na Peru walitoka sare ya 1-1 mjini Lima, wageni wakitangulia kwa bao la James Rodriguez ambaye alipewa pasi na Falcao mwenyewe.
  Radamel Falcao (kushoto) anadaiwa kuwarubuni wachezaji wa Peru wasiifunge Colombia mechi ya kufuzu Komne la Dunia PICHA ZAIDI GONGA HAPA 


  Baada ya kupata bao lao, wachezaji wa Peru wakaendelea kucheza kwa nguvu kabla ya Falcao kuwafuata kuwaambia wapunguze makali mechi iishe kwa sare.
  Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United na Chelsea alionekana kuwasogelea wachezaji wa Peru mmoja mmoja kuwapa ujumbe huku akionekana kumsukuma mchezaji mwingine akampe ujumbe na mwenzake.
  Na tangu hapo mchezo ukapooza kutokana na dhamira ya kucheza uishe kwa sare kama ulivyomalizika kwa timu hizo kufungana 1-1.
  Na kwa matokeo hayo, Colombia imefuzu moja kwa moja Kombe la Dunia wakati Peru watakwenda kwenye mchujo wa kuwania kwenda Urusi mwakani na watamenyana na New Zealand nyumbani na ugenini mwezi ujao.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FALCAO ADAIWA KUWARUBUNI WACHEZAJI PERU WAPANGE MATOKEO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top