• HABARI MPYA

  Monday, June 19, 2017

  TAIFA STARS YAANZA KUJIFUA KWA COSAFA

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  KIKOSI ch timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo kimeanza mazoezi Uwanja wa kituo cha Jakaya Mrisho Kikwete (JMK), eneo la Gerezani, Dar es Salaam kujiandaa na michuano ya Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika (COSAFA) Castle nchini Afrika Kusini baadaye mwezi huu.
  Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas ameiambia Bin Zubeiry Sports - Online leo kwamba, Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti ilifanya mazoezi ya asubuhi Uwanja wa JMK na jioni itahamia Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  “Hali za wachezaji wote ni nzuri baada ya daktari wa timu ya taifa kuwafanyia vipimo vya afya jana walipowasili tu kambini kwenye hoteli ya Urban Rose iliyopo iliyopo eneo la Kisutu, Dar es Salaam,”.
  Lucas amesema kikosi cha Taifa Stars kinatarajiwa kuondoka nchini Juni 22 kwenda Afrika Kusini kushiriki michuano ya COSAFA kama wa waalikwa kwa mwaka wa pili mfululizo na mara ya tatu kwa ujumla kihistoria. 
  Michuano ya Kombe la COSAFA inatarajiwa kuanza Juni 25, mwaka huu na Tanzania imepangwa kundi A pamoja na Mauritius, Malawi na Angola wakati Kundi B lina timu za Msumbiji, Shelisheli, Madagascar na Zimbabwe. 
  Botswana, Zambia, Namibia, Lesotho na Swaziland na wenyeji, Afrika Kusini zitacheza mechi maalumu za mchujo kuwania kuingia robo fainali.
  Kikosi cha Taifa Stars kilichoingia kambini ni makipa Aishi Salum Manula  (Azam FC), Benno David Kakolanya  (Yanga SC) na Said Mohammed Said (Mtibwa Sugar FC). 
  Mabeki ni Shomary Salum Kapombe (Simba SC), Hassan Kessy (Yanga SC), Gardiel Michael (Azam FC), Hamim Abdulkarim (Toto Africans FC), Erasto Nyoni  (Azam FC), Salim Mbonde, (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Nurdin Chona (Tanzania Prisons).
  Viungo ni Himid Mao (Azam FC), Salmin Hoza wa Azam FC, Muzamil Yassin (Simba), Simon Msuva (Yanga SC), Raphael Daudi (Mbeya City) na Shizza Kichuya (Simba SC).
  Washambuliaji ni Thomas Ulimwengu (AFC Eskilstuna – Sweden), Mbaraka Yussuf (Azam FC), Stahmili Mbonde (Mtibwa Sugar), Elius Maguli (Dhofar SC) na Shabani Idd Chilunda (Azam FC).
  Benchi la Ufundi linaundwa na Salum Mayanga, akisaidiwa na Fulgence Novatus, kocha wa makipa, Patrick Mwangata, Meneja Dani Msangi, Madaktari Gilberti Kigadiya na Richard Yomba pamoja na mtunza vifaa Ally Ruvu.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS YAANZA KUJIFUA KWA COSAFA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top