• HABARI MPYA

  Saturday, May 06, 2017

  JKT RUVU YAIPA MKONO WA KWAHERI LIGI KUU, AZAM YAIPUNGUZA KIBURI MBAO

  Na Mwandishi Wetu, MWANZA
  RASMI JKT Ruvu imeipa mkono wa kwaheri Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa wenyeji, Toto Africans jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
  Matokeo hayo yanaifanya JKT iliyopanda Ligi Kuu mwaka 2002 imefikisha mechi 28 ikiwa na pointi 23 ambazo haziwezi tena kuwabakiza kwenye ligi hiyo.  
  Kwa Toto Africans, baada ya ushindi huo uliotokana na mabao ya mshambuliaji wake hatari, Waziri Junior inafikisha pointi 29 baada ya kucheza mechi 27 na inajivuta juu hadi nafasi ya 14 kwenye ligi ya timu 16, ingawa bado imo ndani ya timu tatu za kushuka Daraja.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, mabingwa watetezi, Yanga wameifunga 2-0 Tanzania Prisons ya Mbeya Uwanja wa Taifa, Azam FC wameichapa Mbao FC ya Mwanza 3-0 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, Ruvu Shooting wamelazimishwa sare ya 1-1 na Kagera Sugar Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani, Pwani na  Maji Maji wameifunga 3-0 Mwadui ya Shinyanga Uwanja wa  Maji Maji, Songea.
  Ligi Kuu itaendelea kwa mchezo mmoja tu kesho, Simba SC ikimenyana na African Lyon Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JKT RUVU YAIPA MKONO WA KWAHERI LIGI KUU, AZAM YAIPUNGUZA KIBURI MBAO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top