• HABARI MPYA

  Saturday, May 06, 2017

  HERRERA MCHEZAJI BORA WA MWEZI APRILI MAN UNITED

  KIUNGO Ander Herrera amechaguliwa Mchezaji Bora wa mwezi Aprili wa klabu ya Manchester United baada ya kiiwango kizuri alichoonyesha.
  Mspaniola huyo amepata asilimia 46 ya kura akimzidi Eric Bailly na Marcus Rashford ambao wote wamepata asilimia 27.
  Herrera alikabidhiwa tuzo yake jana Uwanja wa mazoezi wa Aon Complex baada ya kuwasaidia Wekundu hao kushinda 1-0 nchini kwao, Hispania dhidi ya wenyeji Celta Vigo kwenye Nusu Fainali ya kwanza ya Europa League.
  Ander Herrera baada ya kukabidhiwa tuzo yake jana Uwanja wa mazoezi wa Aon Complex 

  Hii inakuwa mara ya tatu kiungo huyo anashinda tuzo hiyo, baada ya kushinda pia Februari na Aprili 2015.
  Aliikosa kosa pia na tuzo ya Octoba mwaka jana baada ya kuzidiwa kidogo na Mspaniola mwenzake, Juan Mata.
  Herrera amekuwa katika kiwango kizuri siku za karibuni kwenye Ligi Kuu ya England na zaidi aling'ara kwenye mchezo dhidi ya vinara wa ligi hiyo, Chelsea.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HERRERA MCHEZAJI BORA WA MWEZI APRILI MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top